Israel yafanya mashambulizi kusini mwa Lebanon

 

Jeshi la Israel limetangaza mapema Jumamosi kwamba limemuuwa mwanachama mmoja wa kundi la Kipalestina la Hezbollah katika eneo la Froun Kusini mwa Lebanon siku ya Ijumaa 21.11.2025.

Taarifa ya jeshi hilo imeongeza kuwa mtu huyo aliyeuawa alikuwa akiendesha mashambulizi ya kigaidi dhidi ya Israel. Katika tukio jingine, mamlaka za Lebanon zimesema mashambulizi ya Israel yaliyoilenga kambi ya wakimbizi wa Kipalestina ya Ain al-Hilweh Kusini mwa Lebanon mwanzoni mwa juma,  yaliwaua wanamgambo 13 wa Hamas.

Israel yadai kulenga miundombinu ya Hamas kusini mwa Lebanon

Taarifa ya jeshi la Israel imesema mashambulizi hayo yalielekezwa kwa kituo cha mafunzo cha Hamas.  Israel imekuwa ikifanya mashambulizi ya mara kwa mara kusini mwa Lebanon licha ya makubaliano ya kusitisha vita kati ya Israel na Kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran.


Post a Comment

Previous Post Next Post