Mapinduzi ya kijeshi si jambo jipya nchini Guinea-Bissau. Taifa hilo la Afrika Magharibi limewahi kupitia majaribio au mafanikio yasiyopungua tisa ya mapinduzi tangu lipate uhuru kutoka Ureno mwaka 1974.
Lakini pale maafisa wa jeshi walipotangaza kuwa walikuwa wametwaa mamlaka ya nchi Jumatano iliyopita, baadhi ya wachambuzi na wanasiasa walionesha shaka.
Dalili zote za kawaida za mapinduzi zilikuwepo: milio ya risasi ilisikika karibu na ikulu ya rais, Rais Umaro Sissoco Embaló alikamatwa, na wanajeshi wakatoa taarifa kupitia televisheni ya taifa.
Hata hivyo, mazingira mengine ya tukio hilo yameibua maswali, huku Waziri Mkuu wa Senegal Ousmane Sonko na Rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan wakiungana na wengine wanaoamini kuwa kutwaa madaraka huko kulipangwa na Embaló mwenyewe.
Zaidi ya hapo, mambo yalizidi kuwa tata wakati jeshi lilipoambia BBC kwamba limetwaa mamlaka ya nchi, lakini likalaani matumizi ya neno "mapinduzi".
Viongozi wa junta walisema walikuwa wakichukua hatua kuzuia njama ya wanasiasa ambao hawakutajwa majina, waliokuwa na "msaada wa mfanyabiashara maarufu wa dawa za kulevya", ya kutaka kuisumbua nchi ambayo kwa muda mrefu imejulikana kama kitovu cha biashara ya dawa za kulevya.
Nini kilitokea katika kipindi kilichosababisha mapinduzi hayo?
Siku tatu tu kabla ya jeshi kutwaa mamlaka, wananchi wa Guinea-Bissau walikuwa wamepiga kura katika uchaguzi wa rais. Embaló, mwenye umri wa miaka 53, alikuwa akigombea muhula wa pili, na mpinzani wake aliyemkaribia zaidi alikuwa Fernando Dias da Costa.
Dias alikuwa akiungwa mkono na Waziri Mkuu wa zamani Domingos Pereira, ambaye awali alitarajiwa kugombea urais kwa niaba ya chama kikuu cha upinzani, PAIGC. Hata hivyo, Pereira alizuiwa kushiriki katika kinyang'anyiro hicho baada ya mamlaka kusema kuwa aliwasilisha nyaraka zake kwa kuchelewa
