Zungu spika mpya wa bunge

 

DODOMA: Mbunge Mteule wa Jimbo la Ilala, Dar es salaam Mussa Azzan Zungu ameibuka mshindi wa kinyang’anyiro cha Kiti cha Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Zungu amechaguliwa kwa kupata kura 378 dhidi ya Wapinzani wake Veronica Charles Tyeah wa Chama cha NFA ambaye hajapata kura, Anitha Alfan wa Chama cha NLD aliyepata kura moja, Ndoge Said Ndonge wa AFP aliyepata kura moja pamoja na Amin Alfred Yango wa ADC ambaye hajapata kura.

Post a Comment

Previous Post Next Post