DODOMA : WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo wameapishwa kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Shughuli hiyo ya uapisho imefanyika mbele ya Spika wa Bunge, Mussa Azzan Zungu, katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma. Wabunge hao wamekula kiapo cha uaminifu na utiifu kwa Katiba na kuahidi kutekeleza majukumu yao kwa maslahi ya Taifa.
Tags
Habari za Kitaifa
