Akizungumza mkoani Simiyu, Makolobela amesema kwa mwaka wa fedha uliopita, ofisi yake ilipewa lengo la kukusanya Sh bilioni 4, lakini walifanikiwa kukusanya zaidi ya Sh bilioni 4.5.
Kwa mwaka huu wa fedha tumewekewa lengo la kukusanya Sh bilioni 4.76, na hadi kufikia robo ya kwanza tayari tumekusanya zaidi ya Sh bilioni 1.23, sawa na asilimia 103 ya lengo la robo mwaka,” amesema Makolobela.
Ameongeza kuwa tangu kuanza kwa Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, makusanyo ya madini kupitia wachimbaji wadogo mkoani humo yamefikia zaidi ya Sh bilioni 17, hatua inayodhihirisha ukuaji na uimara wa sekta hiyo katika Mkoa wa Simiyu.
“Kama Mkoa huu utafanyiwa utafiti wa kina, kuna uwezekano mkubwa wa kugundulika mashapo mengine, hususan madini ya metali yanayoweza kuchimbwa kwa kiwango cha kati na kikubwa, hivyo kuinufaisha Serikali na wananchi kwa ujumla,” amesema Makolobela.
Katika hatua nyingine, ameeleza kuwa Mkoa wa Simiyu una vituo vitano vya ununuzi wa madini pamoja na Soko Kuu la Madini lililopo Bariadi Mjini, ambapo shughuli kuu za biashara ya madini zinafanyika kwa ufanisi mkubwa



