China yaufikisha mzozo wake na Japan Umoja wa Mataifa

 

China imeuambia Umoja wa Mataifa kuwa, itaitumia haki yake ya kujilinda kama Japan itajaribu kuiingilia kijeshi kutokana na mzozo juu ya Taiwan unaoendelea kuongezeka kati ya mataifa hayo mawili.

Mwakilishi wa China katika Umoja wa Mataifa Fu Cong kupitia barua yake kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amesema kauli ya hivi karibuni iliyotolewa na Waziri Mkuu wa Japan Sanae Takaichi inakiuka pakubwa sheria ya kimataifa na kanuni za kidiplomasia.

Kauli ya Takaichi ilivyoibua mzozo

Itakumbukwa kuwa hivi karibuni Takaichi alisema kuwa mashambulizi yoyote ya kijeshi ya China dhidi ya kisiwa kinachojitawala cha Taiwan yanaweza kusababisha kitisho kikubwa dhidi ya nchi yake, hali itakayoilazimu Japan kuitumia vilivyo haki yake ya kujilinda. Kauli hiyo ya Novemba 7, imeibua mzozo mkali wakidiplomasia kati ya Japan na China. Taiwan iko kilometa 60 kutoka Japan, na China inalichukulia eneo hilo kuwa sehemu ya himaya yake.

Post a Comment

Previous Post Next Post