GUINEA : ZAIDI ya mashabiki 50 wa soka wamekufa katika mkanyagano kusini mwa Guinea wakati vikosi vya usalama vilipokuwa vikijaribu kutuliza vurugu wakati wa mechi ya soka kwenye uwanja uliokuwa umefurika watazamaji.
Mkanyagano huo ulitokea wakati watu walipojaribu kutoka uwanjani humo, huku wengi wao wakiruka uzio mrefu kuepuka vurugu hizo.
Mechi hiyo iliyochezwa mwishoni mwa wiki hii katika mji wa Nzerekore ilikuwa ni fainali kati ya timu za Labe na Nzerekore na ilikuwa ni kwa heshima ya kiongozi wa kijeshi wa Guinea, Mamadi Doumbouya.
Tags
Michezo
