Tanzania kuna dagaa wa aina mbalimbali wanaovuliwa katika maziwa na baharini. Kimsingi, kukaushwa, kuokwa, kukaangwa na kuanikwa kwa dagaa hao hulenga kuzuia kuharibika, kuongeza mvuto wa kula na hata kumfikia mlaji aliye mbali bila kuharibika na hasa kwa kuzingatia usafi na uhifadhi. Hatua hizi hulenga kue[1]pusha unyevu na bakteria wanaoweza kuathiri vibaya ubora wa dagaa.
Ukaushaji wa dagaa hufanyika kwa njia mbalimbali katika mwambao wa Ziwa Victoria na maziwa mengine. Ukaushaji dagaa husaidia jamii kupata lishe, mapato na kuchangia usalama. Kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Uvuvi ya Mwaka 2015, sekta ya uvuvi ina mchango mkubwa kuongeza usalama wa chakula, mapato ya familia, ajira na kuchangia ukuaji uchumi.
Sekta hiyo huchangia asilimia 1.8 ya pato la taifa na kutoa ajira zaidi ya milioni 6 kwa Watanzania. Utafiti uliofanywa na mwanafunzi wa shahada ya uzamivu katika Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) mwaka 2016, Thomas Nkondola alibaini uwepo wa kiasi kikubwa cha bakteria kwenye dagaa wanaoanikwa na kuhifadhiwa kwa njia za asili.
Njia hizo ni dagaa kuanikwa juu ya mawe, vichanja na kisha kuhifadhi kwenye magunia. Kwa mujibu wa uta[1]fiti huo, njia hizo za asili huruhusu kuwapo unyevu na hatimaye kusababisha ukungu na uchungu jambo ambalo si salama kwa walaji.
Mkazi wa Kayenze Ndogo, jijini Mwanza, Kabula Shinje anasema dagaa ni mboga rahisi kupata kwa kuwa inauzwa kwa bei nafuu na kwamba ni chakula cha kila siku kwa familia yake. Kuhusu madhara ya dagaa kukaushwa juani, ni pamoja na kuwa na mchanga na ladha ya uchungu na kwamba kuepuka hayo, huamua kununua walio[1]kaangwa.
Anashauri wakaushaji wa dagaa kuhakikisha wanakausha vizuri bidhaa hiyo ya kitoweo kwa kuzingatia usafi, ubora na usalama wa watumiaji. Getrude Mholya yeye anasema dagaa wa Mwanza wana mchanga kwa sababu ya uanikaji wao hivyo hali hiyo humlazimu kukata vichwa na kuosha kwa maji ya moto ili kuondoa mchanga.
Anasema ndio maana hupendelea kuagiza dagaa kutoka Bukoba ili kuondokana na adha hiyo. Katika mwalo huo wa Kayenze Ndogo katika Ma[1]nispaa ya Ilemela, Mwanza, wachakataji wa dagaa hutumia njia tatu kukausha bidhaa hiyo. Anataja njia hizo kuwa ni kuanika juu ya mawe, katika vichanja vya miti na wen[1]gine kutumia teknolojia ya kitalu nyumba kinachotumia nishati ya umeme jua.
Uanikaji wa dagaa juani Sababu ya kutumia mawe ni kwamba yanapatikana kwa urahisi, hawahitaji gharama za ziada na hu[1]wawezesha kuanika dagaa wengi kwa wakati mmoja. Hata hivyo, mawe hupunguza ubora wa dagaa kwani uanikaji wake hauzingatii usafi kwa hiyo hupata vumbi, mchanga na bakteria hatari kwa walaji.
Hali hiyo hufanya dagaa kuuzwa kwa bei ndogo, kutokidhi mahitaji ya soko na badala yake huwa chakula cha mifugo wakiwemo kuku. Wakati wa mvua hali huwa ngumu kwa sababu hawawezi kuanika dagaa juani. Editha Shida anasema anapendelea kuanika kwe[1]nye mawe kwa sababu ana uwezo wa kuanika hadi ndoo 20 kwa wakati mmoja na pia hahitaji gharama za kulipia kichanja ambacho huanzia Sh 3,000 kwa siku au mtambo wa kukaushia dagaa kwa umeme jua.
Mrisho Yusuf anasema anakausha dagaa kwenye mawe kuuzia wanaohitaji vyakula vya mifugo wakiwemo kuku. Anasema yapo baadhi ya maeneo katika baadhi ya mikoa ukiwamo Tabaro ambayo baadhi ya watu wanapendelea dagaa wenye mchanga kwa kuwa huzwa bei nafuu ikilinganishwa na wanaoanikwa kwenye chanja wanaouzwa kwa Sh 3,000 hadi 6,000 kwa ndoo ya lita 20.
Hata hivyo, uanikaji wa dagaa juani unachangamoto zake ikiwemo kupata hasara wakati wa mvua. Aina nyingine ya uanikaji dagaa kwenye mwalo wa Kayenze ndogo ni kwenye vichanja vya miti ambavyo huwekewa nyavu kwa juu kuna mzunguko mzuri wa hewa unaowezesha dagaa kukauka vizuri, kuwa na rangi yao na harufu nzuri.
Kwa mtu anayehitaji kichanja kukaushia dagaa wake, hulazimika kukodi kichanja ama kwa mwezi au siku kwa Sh 3,000 kwa kichanja kimoja. Wenyeji wa mwambao wa ziwa wanasema hupenda njia hii ni kwa sababu hutumia jua la moja kwa moja hivyo, linapokosekana dagaa hawawezi kukauka na badala yake huharibika. Anania Musa yeye anasema kipindi cha mvua uanikaji dagaa kwenye mawe ni changamoto kwa sababu hawawezi kukauka na hivyo huharibika na kuoza.
“Kipindi cha mvua hasara ni kubwa kwa sababu unaweza kununua kwa bei kubwa na ukaishia kuuza kwa bei ndogo, la[1]kini bado tunapata kipato,” anaeleza. Akizungumzia athari za ukaushaji dagaa kwa njia za asili, Ofisa Lishe Mwandam[1]izi, Walbert Mgeni anasema uanikaji wa dagaa kwenye miamba (mawe) au kwenye mchanga si salama kwani mchanga humsababishia mlaji ugonjwa wa kidole tumbo. Pia, anasema kuanika eneo la wazi kwa ujumla kuna hatari ya dagaa kupata minyoo inayoweza kusa[1]babisha magonjwa ya kuhara na homa ya matumbo.
Hii ni kwa kuwa nzi wanapotua hueneza mayai ya minyoo wanayobeba ardhini na kueneza sehemu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kwenye dagaa hao wanapotua juu yake. Mgeni anasema, “Hivyo utaona uwezekano wa kupata magonjwa haya ni mkubwa tofauti na wale wanaotumia teknolojia kukaushia dagaa, maana wanazingatia usafi na pia hakuna wadudu wala ndege wanaoweza kupenya hivyo wanabaki na virutubisho vyote.”
Alipendekeza jitihada ziongezwe kuhamasisha ukaushaji wa dagaa kwa kutumia teknolojia ya kisasa kuongeza ubora na usalama wa chakula. Matumizi ya umeme jua Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003, kifungu cha 24 kinasema Waziri ataweka masharti ambayo ni muhimu kuhakikisha haki ya watumiaji samaki na mazao ya uvuvi iki[1]wemo dagaa, kuwa salama, yenye afya na yasiyoghushiwa.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega anasema dagaa ni zao la kimkakati hivyo, wame[1]anza kutekeleza mikakati ya kupunguza upotevu na kuhakikisha ubora na usalama wake. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta cha nchini Kenya, dagaa waliokaushwa kwa kutumia mitambo ya nishati ya umeme jua ni bora na hawana kiwango cha unyevu unaoweza kuten[1]geneza fangasi wala bakteria ikilinganishwa na njia za asili
