RPC Geita aonya matapeli tiba asili

 

GEITA; JESHI la Polisi mkoani Geita limesema limejizatiti kuhakikisha linakomesha vitendo vya utapeli, ukatili wa kijinsia na ramli chonganishi vinavyofanywa na watu mbalimbali kwa kivuli cha tiba za asili.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), Safia Jongo ametoa kauli hiyo katika mkutano mkuu wa waganga wa tiba za asili mkoani Geita uliofanyika mjini Geita..

Amesema hatua hizo zinakuja kutokana na kuendelea kuripotiwa matukio ya vitendo  visivyo vya kiungwana, vinavyofanywa na baadhi ya waganga wa tiba za asili.

Amesema hatua kubwa ya kwanza ni kuhakikisha waganga wote wa tiba za asili wanasajiliwa na kisha kuwafuatilia, kuwasaka na kuwakamata wanaodaiwa kutoa tiba za asili, huku hawataki kusajiliwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post