MGOMBEA wa nafasi ya uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Democratic Party (DP), Chrisant Ndege ameahidi kuligeuza Bunge hilo kuwa la maendeleo kwa kufanya kazi inayotokana na bajeti zitakazowasilishwa bungeni na Serikali ambayo malengo yake ni kuwaletea wananchi maendeleo.
Ameyasema hayo bungeni Dodoma leo wakati akiomba kura kwa wabunge za kumchagua kuwa Spika. Pia ameahidi endapo atachaguliwa kuwa spika atalisimamia Bunge kuhakikisha miswada yote ya sheria inayowasilishwa bungeni kupitishwa kuwa sheria inazingatia maadili ya kitanzania na si vinginevyo.
Tags
Habari za Kitaifa
