ARUSHA: Mashindano ya Ligi ya Vijana wenye umri chini ya miaka 13 yanatarajiwa kuendelea kesho Novemba 8 kwa michezo minne itakayochezwa katika viwanja vya Shule ya Kimataifa Kennedy House, Usa River Wilaya ya Arumeru.
Jumla ya timu 8 zinashiriki ligi hiyo iliyoandaliwa na kituo cha kukuza soka kwa vijana cha ‘Young Boys Academy’ kilichopo Arumeru mkoani Arusha.
Michezo minne itachezwa ambapo mechi ya kwanza itazikutanisha timu za Satino Academy dhidi ya timu ya Follow Your Dream Academy mchezo utakaoanza saa nne asubuhi.
Tags
Michezo
