WANANCHI wa Jimbo la Same Magharibi wamemshukuru Mbunge wa jimbo hilo, Dk, David Mathayo kwa kusaidia vifaa mbalimbali ikiwemo utatuzi wa kero za maji.
Shukrani hizo wamezitoa na wananchi hao akiwemo Salim Mdee baada ya mbunge huyo kufanya ziara maeneo mbalimbali ya jimbo hilo ikiwemo utoaji wa fedha za umaliziaji ujenzi wa msikiti, mabomba ya maji vifaa vingine vimeelekezwa katika sekta muhimu kama elimu na afya.
Katika ziara yake ya kutembelea kata 20 za jimbo la Same Magharibi, Dk,Mathayo amekuwa akitimiza ahadi zake kwa vitendo na kuongeza kuwa msaada huu ni sehemu ya jitihada zake za kutatua changamoto zinazowakumba wananchi wa jimbo hilo, kama alivyoeleza wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo.
Tags
Habari za Kitaifa


