Tanzania yawekeza huduma waraibu dawa za kulevya

 

TANZANIA imewekeza zaidi katika eneo la kinga kwa kujenga vituo mbalimbali vya kutolea huduma za waraibu wa dawa za kulevya katika hospitali za kanda na rufaa sanjari na utoaji elimu kwa makundi mbalimbali ikiwemo klabu za vijana mashuleni.

Aidha nchi za Umoja wa Afrika zimejitahidi kupunguza vifo vinatokona na matumizi ya dawa za kulevya yaliyopitiliza kwa asilimia 12 kutokana na kazi kubwa ya uhamasishaji kwa jamii dhidi ya matumizi ya dawa hizo.

Hayo yamesemwa Jijini Arusha na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera,Bunge na Utaratibu), Ummy Ndeurananga kwaniaba wa Waziri wa Afya, Jenista Mhagama wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa siku nne wa Mashauriano ya Umoja wa Afrika na Muungano wa Kimataifa kuhusu Kupunguza Uhitaji wa Dawa za Kulevya kwakushirikiana chini ya wenyeji kutoka Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA).

Amesema mafanikio hayo yametokana na kasi inayofanywa na Rais, Samia Hassan Suluhu katika uwekezaji kwenye vituo vya waathirika wa dawa za kulevya katika hospitali za Kanda na Rufaa nchini sanjari na kuongeza zaidi utoaji wa elimu kwa makundi mbalimbali kwakushirikiana na ofisi ya DCEA.

Amesema serikali inaendelea kudhibiti matumizi ya dawa za kulevya mitaani ikiwemo kuhakikisha wanaokamatwa na dawa za kulevya wanachukuliwa hatua stahiki lakini pia Tanzania imeanzisha kituo cha utoaji huduma(call centre) kwakupiga simu na kutoa taarifa mbalimbali za kudhibiti matumizi ya dawa hizo.

Wakati huo huo, Naibu Katibu Msaidizi, Mipango, Sera za Kimataifa anayeshughulikia Ofisi ya Afrika na Mashariki ya Kati katika Masuala ya Kimataifa ya Utekelezaji wa Sheria,(INL), Maggie Nadri alisema vifo vinavyotokana na matumizi ya dawa za kulevya yaliyopitiliza vimepungua kwa asilimia 12 katika nchi za Umoja wa Afrika huku alisistiza kuongeza nguvu zaidi katika mapambano hayo ya dawa hizo ikiwemo utoaji wa elimu kupitia klabu za vijana mashuleni

Post a Comment

Previous Post Next Post